TIMU YA IRINGA ALL STARS VETERAN WAAHIDI KUCHUKUA KOMBE LA BONANZA LITAKALOFANYIKA JIJINI DODOMA

Timu ya Iringa All Star Veteran (IASV) ya mjini Iringa imejipanga vyema kuibuka kifedha katika bonanza litakalofanyika jijini Dodom likaloshirikisha timu 24 kutoka mikoa nane ya Tanzania Bara, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Akizungumza katika mazoezi ya mwisho yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Mkwawa, nahodha wa timu hiyo, Lissa Mwalupindu amesema kuwa, wachezaji wote wa timu hiyo wamefanya mazoezi na wapo timamu kuhakikisha wanaibuka mabingwa kwenye bonanza hilo.

Amesema kuwa, timu hiyo ina wachezaji wengi wazoefu na wana uwezo mkubwa wa kucheza mpira na kupata ushindi kwenye bonanza hilo.
Timu ya Iringa All Star Veteran (IASV) ya mjini Iringa ikiwa imetoka katika mechi ya kujiandaa kwa ajili ya bonanza litakalofanyika jijini Dodoma likaloshirikisha timu 24 kutoka mikoa nane ya Tanzania Bara.

"Timu hii ina wachezaji wengi waliocheza ligi kuu, ligi daraja la kwanza, la pili na ngazi ya mkoa ambao wamefanya mazoezi kwa muda mrefu na wamekubaliana kurudi na kombe hilo mkoani Iringa, ili kutoa hamasa kwa vijana kuwa na ari ya ushindani kupitia wao kama kioo,"amesema.

Amwsema kuwa, bonanza hilo litakaloshirikisha timu kutoka mikoa nane ambayo ni Pwani, Iringa, Dar es Salaam, Morogoro, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na wenyeji Dodoma.

Nao wachezaji wa timu hiyo Davis Wapalila na Abissay Stesheni Jr walitoa onyo kwa timu binzani kujipanga kwa kuwa timu hiyo ipo timu na inaenda kuchukua kombe na sio kushiriki bonanza hilo.

"Sisi wachezaji tupo sawa kweli kweli na tumejipanga kuhakikisha tunaibuka kuwa mabingwa wa bonanza hilo ambalo kwa mara ya kwanza limezikutanisha timu nyingi kutoka mikoa nane ya Tanzania Bara,"wamesema.

Naye msemaji wa timu hiyo ya Iringa All Star Veteran, Denis Mlowe ametoa tahadhari kwa timu pinzani wajipange kweli kweli kwa kuwa timu ya Iringa all stars veterani wana timu ya ushindani na wamefanya mazoezi muda mrefu na wamejipanga kushinda kombe hilo la bonanza hilo.

"Hawa wazee wako vyema kuhakikisha wanatoa dozi kwa timu yoyote hivyo lengo ni kushinda bonanza hilo ambalo tumelichukulia umuhimu mkubwa na kuwafundisha vijana jinsi ambavyo tulikuwa tunacheza zamani,"amesema.

Kwa upande wake Mratibu wa timu hiyo ya Iringa all stars veterani, Adv.Lupyana Massawa amesema kuwa wachezaji wote wa timu hiyo watakuwepo kwenye bonanza hilo isipokuwa wachezaji watatu waliopata majeruhi ambao ni Humphrey Ndale, Yohana Tembe na Petro Mrope lakini wachezaji wengine wote wapo vizuri kabisa kwa ajili ya bonanza hilo

Aidha, Massawa ameongeza kuwa, wachezaji watakaosafiri na timu ni:

1. Attanas Maginga, 2. Adv. Evalisto Myovela, 3. Lissa Mwalupindi, 4. Tumaini Abbisai Stephen, 5. Pendo Mapunda, 6. Abuu Silia, 7. Ally Ngalla, 8. Steve Lihawa, 9. Omary Daudi, 10. Hasan Ussi, 11. Rashid Msigwa, 12. Ally Msigwa, 13. Dikson Kiboye, 14. Denis Mlowe, 15.Khalid Fungabrek, 16.Pendo Mapunda, 17. Nicholaus Shari, 18.Petro Mrope, 19.Fredy Mgunda, 20.Davis Wapalila, 21.Ramadhani Shemhilu,22. Godlisten Mlaki,23.Ally Lwambano,24.Lusekelo Kibona, 25.Simba Yusuph.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news