|
Ni kama Tundu Lissu inaonekana amepangua madai ya Kamati ya Taifa ya Maadili ambayo imeeleza hivi leo, "Leo Oktoba 2, 2020 Kamati ya Maadili
ya Kitaifa imesikiliza malalamiko dhidi ya Mgombea wa Kiti cha Rais
kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.
Malalamiko
yaliwasilishwa na Chama cha NRA na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Chama cha
NRA wakilalamikia kitendo cha mgombea wa kiti cha kiti cha Rais kupitia
CHADEMA kutoa maneno ya uchochezi yasiyothibitika;
Katibu wa
Kamati ya Maadili ya Kitaifa, Emmanuel Kawishe ameyabainisha haya leo
Oktoba 2, 2020 baada ya wajumbe wa kamati kukutana, anaripoti Mwandishi Diramakini (diramakini@gmail.com).
"Ambapo
akiwa mkoani Mara, alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, John Pombe Magufuli ameitisha kikao cha wasimamizi wa uchaguzi
nchi nzima ili kuhujumu uchaguzi. Pia imeelezwa kuwa alitoa maneno ya
kichochezi na ya kudhalilisha kinyume na maadili ya uchaguzi mkoani
Geita,"amaefanua. Baada ya uamuzi huo Lissu naye amejibu kupitia ukuta wake wa Twitter kama ifuatavyo hapa chini.
|
"Mchana huu Kamati ya Maadili imenisimamisha kufanya kampeni kuanzia kesho.Uamuzi huu sio wa kushangaza hata kidogo.Naomba nizungumze juu ya utaratibu ambao umefanyika.
1. Hadi sasa sijapatiwa tuhuma yoyote ya malalamiko ya mgombea yoyote au chama chochote kuhusu ukiukaji wa maadili yoyote. Sina taarifa yoyote ya maandishi kinyume cha utaratibu.
2. Sijapewa fursa yoyote ya kuwasilisha utetezi wa maandishi. Maadili yanasema ikitokea kuna malalamiko, anatakiwa apeleke kwa tume na mtuhumiwa apewe nakala na apewe masaa 42 ya kujibu.
3. Hadi sasa hakuna wito wowote wa kwenda kwenye kikao cha Kamati ya Maadili.
4. Nimepokea kama ninyi mlovyopokea kwa kupitia vyombo vya habari ambayo ni kinyume cha utaratibu,"amefafanu Lissu.