Vijana, wanawake, watu wenye ulemavu Geita Mji wapatiwa milioni 233/-

Halmashauri ya Mji wa Geita kutoka katika mapato yake ya ndani imetoa shilingi milioni 233 kwa vikundi 49 vya vijana,wanawake na watu wenye ulemavu, anaripoti Robert Kalokola (Diramakini), Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel (wa pili kutoka kulia) akikabidhi hundi ya shilingi milioni 233 kwa wa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Halmashauri ya Mji wa Geita. (DIRAMAKINI).
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi kwa vikundi hivyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita, Mhandisi Modest Apolinary amesema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2020/2021 wametenga jumla ya shilingi 735,987,571 ikiwa ni asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya vikundi vya vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.

Mhandisi Modest Apolinary amesema kuwa, wametoa mikopo kwa makundi hayo kwa vikundi vya vijana wamepewa mkopo wa shilingi 107,000,000 ,vikundi vya wanawake shilingi 123,000,000 na watu wenye ulemavu shilingi 3,000,000.

Aidha , Mhandisi Modest Apolinary ameongeza kuwa, katika kipindi cha mwaka 2017-2020 halmashauri hiyo imeshatoa mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali jumla ya shilingi bilioni 2.5 kwa miaka minne.
Baadhi ya wanawake walioshiriki hafla ya kupokea mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu jumla ya shilingi milioni 233 kutoka Halmashauri ya Mji wa Geita. (DIRAMAKINI).
Mhandisi Modest Apolinary ameongeza kuwa, kuanzia mwaka wa fedha Julai Mosi mwaka 2020 halmashauri hiyo imeshakusanya mapato ya ndani shilingi Bilioni 2.1 kwa miezi mitatu tu.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akikabidhi hundi kwa vikundi hivyo vya wajasiriamali amewasihi kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ili iweze kuwasaidia kukuza vipato vyao.

Amewataka kukumbuka kurejesha fedha hiyo ili makundi mengine yaweze kukopa ili kufanya shughuli zao za kukuza uchumi.
Mkuu wa Mkoa wa Geita , Mhandisi Robert Gabriel (wa pili kutoka kulia) wa kwanza ni Mkuu wa Wilaya ya Geita, Fadhili Juma,Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu (wa pili kutoka kushoto) wakiwa kwenye hafla ya kutoa mikopo kwa wajasiriamali katika Halmashauri ya Mji wa Geita. (DIRAMAKINI).
Naye Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amemshukuru Mkurugenzi wa mji wa Geita kwa kuendelea kutekeleza mpango huo wa kutoa mikopo kwa vijana, wanawake pamoja na walemavu hata baada ya baraza la madiwani kuvunjwa.

Kanyasu amesema kuwa,hutoaji wa mikopo hiyo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015-2020.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news