WAHANDISI KUTOKA BODI YA USAJILI WA WAHANDISI NCHINI WAKAGUA UJENZI WA DARAJA LA KIGONGO-BUSISI



Muonekano wa mtambo wa kuchanganya zege itakayotumika katika ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi lenye urefu wa kilomita 3.2 linalojengwa mkoani Mwanza.

Msajili wa Wahandisi nchini, Mhandisi Patrick Barozi amesema Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), itaendelea kusambaza wahandisi wake katika miradi mikubwa ya ujenzi inayoendelea nchini ili kuwajengea uwezo na uzoefu wa kuisimamia miradi hiyo itakapokamilika,anaripoti Mwandishi Diramakini.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi lenye urefu wa kilomita 3.2 na barabara unganishi zenye urefu wa kilomita1.66,Mhandisi Barozi amesisitiza umuhimu wa wahandisi wanaopata fursa katika ujenzi wa miradi mikubwa na yakimkakati hapa nchini kujitahidi kuwa na bidii na nidhamu ili kupata ujuzi zaidi utakaorithishwa kwa vizazi vijavyo.

Msajili wa Wahandisi nchini,Mhandisi Patrick Barozi (wapili kushoto), akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Bw.Juma Sweda (kushoto), mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi lenye urefu wa kilomita 3.2.
“Fahamuni ninyi ni mabalozi wetu kwenye miradi hii, hivyo bidii yenu itawawezesha kujifunza mengi na hivyo kuiwezesha nchi kumudu kujenga miradi kama hii hapo baadae,”amesisitiza Mhandisi Barozi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Misungwi linakojengwa daraja hilo, Bw.Juma Sweda amewataka wakazi wa wilaya hiyo kutumia fursa hiyo kufanya biashara na kupata ajira ili kukuza uchumi wao.

Msajili wa wahandisi nchini, Mhandisi Patrick Barozi akisisitiza jambo kwa wahandisi waliopata fursa katika mradi wa ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi lenye urefu wa kilomita 3.2 kujifunza kikamilifu ili kupata ujuzi wa kutosha katika ujenzi huo.

Kazi ya ujenzi wa daraja la muda litakalotumika katika kuwezesha kupitisha vifaa wakati wa kujenga daraja la kudumu la Kigongo-Busisi lenye urefu wa kilomita 3.2 ikiendelea.

Kazi ya ujenzi wa daraja la muda litakalotumika katika kuwezesha kupitisha vifaa wakati wa kujenga daraja la kudumu la Kigongo-Busisi lenye urefu wa kilomita 3.2 ikiendelea.

Kaimu meneja mradi wa ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi lenye urefu wa kilomita 3.2,Mhandisi Abdulkarim Majuto akifafanua jambo kwa timu ya wahandisi toka Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini (ERB) walipokagua ujenzi huo.
Amesema, kuwepo kwa ujenzi huo wa miaka minne kukitumiwa vizuri na wananchi kutawapa ajira na biashara nzuri hivyo ni wakati wao kuchangamkia fursa hiyo.

Kaimu Meneja Mradi huo,Mhandisi Abdulkarim Majuto amesema wamejipanga kuhakikisha watanzania wanapata fursa za ujuzi na waliopata ajira wanalipwa maslahi bora ili daraja hilo liendelee kuleta neema kwa wananchi.

Daraja la Kigogo-Busisi lenye urefu wa kilomita 3.2 linalojengwa na kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) na China Railway 15 Bureau Group Corporation zote za China linaelezwa kuwa la sita kwa urefu barani Afrika na linatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 669 litakapokamilika.

Timu ya wahandisi kutoka Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), wakifuatilia maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi lenye urefu wa kilomita 3.2 linalojengwa mkoani Mwanza kutoka kwa kaimu meneja mradi huo Eng. Abdulkarim Majuto hayupo pichani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news