Ni Oktoba 3,2020 iliyoacha alama ambapo kila mwananchi aliyezungumza na Mwandishi Diramakini katika Jiji la Arusha kauli yake ilikuwa shukurani tu."Asante Rais Dkt.John Magufuli, asanteni Shirika la Reli Tanzania (TRC) mmetuheshimisha mno, baada ya miaka 30 bila treni, hatimaye leo...Mungu awabariki kwa kazi nzuri," hayo ni maneno ya shukurani kutoka kwa wananchi.
“Kwa kweli siamini hiki ninachokiona, namshukuuru Rais Magufuli nawashukuru TRC wamefanya kazi kubwa kurejesha huduma hii iliyosimama kwa muda mrefu, sasa tutapata fursa za kufanya biashara na shughuli nyingine za kiuchumi,"ameongeza Zubeda Ally kutoka jijini humo.Ni baada ya treni ya abiria kuwasili katika Stesheni ya Arusha jijini humo,ikiwa ni baada ya zaidi ya miaka 30 na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Kenani Kihongosi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na maelfu ya wakazi wa jijini hilo.
Treni hiyo ya abiria iliruhusiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Abubakar Kunenge katika Stesheni ya Kamata jijini Dar es Salaam kuelekea Oktoba 2, 2020.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema kuwa,wamefurahishwa na ujio wa treni hiyo kwani unakwenda kufungua fursa za ajira na biashara kwa wakazi wa jiji hilo.
“Sisi kama wananchi wa jiji wa Arusha tunafarijika sana na ujio wa treni hii, kwa sababu inakwenda kufungua fursa za uchumi kwa jiji letu la Arusha kwa sababu vijana watakwenda kupata ajira na biashara zinakwenda kufanyika,"amesema Kihongosi.
DC Kihongosi ameongeza kuwa,unafuu wa nauli katika usafiri wa treni una faida kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa Arusha na nchi kwa ujumla.
“Kama kwenye basi mtu anaweza kulipa Shilingi 32,000 kwenye treni akalipa 16,000 anaweza kuokoa kiasi cha fedha ambacho kinaweza kusaidia kufanya mambo mengine, kwahiyo hii ni fursa kubwa tunamshukuru na kumuombea sana Mheshimiwa Magufuli," amesema DC huyo.
Pia Kihongosi amewasisitiza wananchi wa Jiji la Arusha kuendelea kuitunza reli ili iweze kuleta manufaa kwa watanzania wote kwa ujumla na kuwataka wananchi kumuunga mkono Rais Magufuli kwa jitihada anazozifanya katika kuboresha sekta ya miundombinu ya reli nchini. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TRC,Prof. John Wajanga Kondoro amemshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa maamuzi yake ya kuwekeza katika uboreshaji wa sekta ya miundombinu ya reli nchini, pia ameahidi kuendelea kusimamia utekelezaji wa maagizo ya Mheshimiwa Rais katika kuboresha sekta ya usafiri wa reli nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli, Masanja Kadogosa ameeleza kuwa, usafiri wa reli katika mikoa ya Kaskazini umerejea na utaendelea kuwepo kwani shirika limeandaa mikakati ya kuboresha huduma ya usafiri katika maeneo hayo kwa kuanzisha huduma ya usafiri wa treni za mjini kati ya Moshi na Arusha ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni na kwa kujenga reli mpya ya viwango vya kimataifa -SGR kuanzia Tanga-Moshi-Arusha hadi Musoma mkoani Mara.
Treni ya abiria ya Deluxe inafanya safari kati ya Dar es Salaam na Arusha siku za Ijumaa na Jumatatu kutoka Dar es Salaam na Jumamosi na Jumanne kutoka jijini Arusha ambapo kwa mwezi Oktoba shirika limetoa ofa ya punguzo la asilimia 15 kwa nauli za treni kwa madaraja yote.
hongeren dira makini mko vizur san
ReplyDelete