Wananchi watajwa uharibifu miundombinu ya maji

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji ambaye anaendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya maji mkoani Kagera, Mhandisi Nadhifa Kemikimba amesikitishwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wananchi wasiokuwa wazalendo kwa nchi yao kwa kuhujumu miundombinu ya miradi ya maji na baadae kuanza kulalamika kuwa hawapati huduma ya maji, anaripoti Allawi Kaboyo, Ngara.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba aliyeinama akikagua moja ya chemba ya kutegea maji ya mradi wa maji wa Kijiji cha Rwinyana wilayani Ngara mkoani Kagera. (DIRAMAKINI).
Mhandisi Nadhifa ameyasema hayo Oktoba 14, mwaka huu alipofika katika Kijiji cha Rwinyana baada ya kupokea malalamiko mbalimbali ya wananchi wa kijiji hicho kuwa hawapati maji na kuamua kwenda kwenye chanzo cha mradi huo ili kuangalia tatizo ni nini na kwa nini wananchi hawapati maji.

Katika safari hiyo ya kuelekea kwenye chanzo hicho cha maji, Naibu Katibu Mkuu ameambatana na baadhi ya wananchi akiwemo mwenyekiti wa kijiji hicho pamoja na wataaamu aliokuwa nao kwenye msafara, mara baada ya ya kufika kwenye chanzo hicho aliridhika na wingi wa maji unaozalisha ambapo alisikitishwa na vitendo vya wananchi kuanzisha kilimo kwenye chanzo hicho na sehemu nyingine kukuta mabomba ya maji yakiwa yamekatwa kwa vitu vyenye ncha kali na kupelekea maji kumwagika kwa kiasi kikubwa.

“Lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wote hasa wa vijijini wanapata huduma ya maji safi, lakini baada ya kufika kwenye mradi huu nimepokea malalamiko ya wananchi kuwa mradi huu hautoi maji na hata yakitoka basi hayakidhi mahitaji huku Serikali ikiwa imetumia fedha nyingi kuutekeleza mradi huu, nilichogundua hapa nyote ni mashaihidi nyinyi wananchi ndio sababu mojawapo ya kutopatikana kwa maji ya uhakika katika kijiji chenu, mmeona hapa mabomba yamekatwa kabisa na maji yanamwagika,"amesema Naibu Katibu Mkuu.

Aidha, kufatia hali hiyo amemuagiza Mhadishi wa Wakala wa Maji Vijijini RUWASA kuanza ukarabati wa mradi huo ambao una miaka saba toka uipoanza kutekelezwa ili uanze kutoa maji ya uhakika kwa wanachi kama ilivyokuwa imekusudiwa kabla ya sikukuu za Krismas za mwaka huu.

Awali akisoma taarifa ya mradi huo, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Ngara, MhandisiAbdi Andaru amesema kuwa, mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2013 na kutarajiwa kukamiika mwaka 2014 huku gharama za mradi huo zikiwa ni shilingi za kitanzania milioni 501 ambapo mkandarasi aitwaye Nyamasirir General Promotion & Supplies amelipwa kiasi zaidi ya shilingi milioni 455.

Akiwa katika wilaya za Missenyi, Kyerwa na Karagwe Naibu Katibu Mkuu alitembelea na kukagua miradi ya maji ya Kijiji cha Bisole upande wa Kyerwa na mradi wa Chabuhola upande wa Wilaya Karagwe ambapo amewaagiza mameneja wa wilaya hizo kuhakikisha wanaibua miradi ambayo itawawezesha wananchi kupata maji kwa ukaribu zaidi kwa kuwa wananchi hao hawajajikusanya sehemu moja.

Domini Kasigwa ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Bisole ambayye ameeleza kuwa kabla ya ujio wa mradi huo walikuwa wakiteseka sana kufuata maji mbali na zaidi walikuwa wakitumia maji ya madimbwi hali iliyowapekea kuhatarisha afya zao kutokana na kutumia maji ambayo sio salama, ambapo ametumia fursa hiyo kuishukuru serikali kwa kuwaletea mradi mkubwa wa maji na sasa wanafurahia maisha.
Mtoto Eliana Leonard akifurahia huduma ya maji katika moja ya DP ambazo zimejengwa katika Kijiji cha Rwinyina. (DIRAMAKINI).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news