Ripoti mpya iliyowasiliswa katika Umoja wa Mataifa inakadiria kuwa wanawake milioni 29 pamoja na wasichana ni wahanga wa utumwa wa kisasa, ambao hulazimishwa kufanya kaz na kuolewa kwa lazima, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kwa mujibu wa mwanzilishi mwenza wa shirika la kupambana na utumwa la Walk Free, Grace Forrest anasema, idadi hiyo inamaanisha kila mwanamke mmoja kati ya 130 wanaishi katika mazingira hayo.
Grace Forrest ameongeza kwamba , makadirio hayo hayajumuishi matukio yaliyojitokeza wakati huu wa janga la virusi vya corona (Covid-19).
Amesema, kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la ndoa za kulazimishwa na ndoa za utotoni katika jamii tofauti duniani kote. Mwanzilishi huyo amesema,Walk Free pamoja na programu ya Umoja wa Mataifa ya Kila Mwanamke Kila Mtoto kwa pamoja wamezindua kampeni ya kimataifa ya kupinga utumwa wa wanawake duniani.
Amesema, kupitia kampeni hiyo wanaamini italeta mabadiliko makubwa zaidi na matokeo yake yatakuwa chanya katika kukomesha utumwa wa namna hiyo.