Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) limeshinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka huu kutokana na juhudi zake za kupambana na njaa, kuboresha mazingira ya mizozo na kuzuia matumizi ya njaa kama zana za kivita na mzozo katika maeneo mbalimbali duniani, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kamati ya Nobel wakati ikitangaza uamuzi wake imesema, imelenga kugeuza jicho la Dunia kwa mamilioni ya watu wanaokabiliwa na njaa na umaskini wa chakula katika pande mbalimbali.
Tangazo hilo limetolewa mjini Oslo na Berit Reiss-Andersesn, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Nobel. Kamati hiyo imesema janga la virusi vya corona (Covid-19) limeongezea tatizo la njaa linalowakabilia mamilioni ya watu kote duniani.
Pia ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa serikali kuhakikisha kwamba WFP na mashirika mengine ya msaada yanapokea msaada wa kifedha unaohitajika kulisha watu hao kwa wakati.
Reiss-Anderesen amesema, WFP inachangia kila siku katika kuendeleza udugu wa mataifa yaliotajwa katika wosia wa Alfred Nobel. Amesema, shirika hilo limekidhi vigezo vyote dhidi ya wagombea kwenye orodha ya mwaka huu ambapo watu 211, mashirika 107 waliteuliwa.
Tuzo hiyo inaambatana na zawadi ya fedha taslimu kiasi cha dola milioni 1.1 pamoja na medali ya dhahabu vinavyotolewa katika sherehe mjini Oslo, Norway, Desemba 10, ambayo ndiyo tarehe ya kukumbuka kifo cha Alfred Nobel. Sherehe ya mwaka huu ilipunguzwa ukubwa kutokana janga la virusi vya corona linaloendelea kuisumbua Dunia.
Msemaji wa WFP, Tomson Phiri amesema, ni jambo la fahari kwa shirika hilo kutambuliwa na tuzo hiyo na kusema hata kuteuliwa tu kuwa kwenye orodha hilo lilikuwa jambo tosha, lakini ushindi ni jambo la kusisimuwa zaidi kwao.

Tags
Kimataifa