Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Innocent Bashungwa ameruhusu uuzaji wa Ethanol nje ya nchi, hayo yemebainishwa leo Oktoba Mosi, 2020 na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Riziki Shemdoe, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu, hatua hii imetokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa Ethanol hapa nchini ambayo inakidhi mahitaji ya ndani na kupatikana kwa ziada inayoweza kuuzwa nje.
"Aidha, Mheshimiwa Waziri amewataka wazalishaji na wasafirishaji wa Ethanol nje ya nchi kuendelea kufuata taratibu zote za kisheria kwa ajili ya kuuza bidhaa hiyo nje ya nchi,"ameeleza Katibu Mkuu Profesa Riziki Shemdoe kupitia taarifa hiyo.