AZAM FC yarejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara

Timu ya Azam FC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo, Azam FC inayofundishwa na Mromania, Aristica Cioaba inafikisha alama 25 baada ya kucheza mechi 10, sasa ikiwazidi alama mbili Yanga SC ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi.

Katika mchezo huo wa Novemba 5,2020 mabao ya Azam FC yamefungwa na Aggrey Morris 47', kiungo mshambuliaji Ayoub Lyanga 58' na beki Hassan Kapona aliyejifunga akijaribu kuokoa kazi nzuri ya kiungo Mzimbabwe, Never Tigere 62'.

Wakati huo huo bao pekee la Hamad Majimengi 56' limetosha kuwapa Coastal Union ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Gairo mkoani Morogoro. Aidha, Mbeya City ikalazimishwa sare ya 1-1 na Polisi Tanzania Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Kibu Dennis alianza kuwafungia wenyeji dakika ya saba, kabla ya Hassan Nassor kuwasawazishia wageni 45'.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news