Baada ya Hifadhi ya Taifa Serengeti kushinda tuzo ya kuwa Hifadhi Bora katika Bara la Afrika kwa mwaka 2020 nayo Bandari ya Dar es Salaam imeibuka kuwa bandari inayoongoza kwa ubora barani Afrika, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Tuzo hiyo ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imetangazwa Novemba 9,2020 na Taasisi ya World Travel Awards (WTA) ya nchini Marekani kwa njia ya mtandao.
Hiyo ikiwa
ni mara ya pili kwa Hifadhi ya Taifa Serengeti kushinda katika Kundi la
Hifadhi zinazoongoza kwa ubora zaidi Bara la Afrika baada kushinda pia
mwaka 2019.
Aidha kwa upande wa bandari, Taasisi ya World Travel Award (WTA) ya London, Uingereza, Jumanne ya wiki hii imeipigia kura Bandari ya Dar es Salaam kuwa Bandari inayoongoza kwa meli za utalii na ubora wa huduma barani Afrika.
Mafanikio haya kwa Bandari ya Tanzania ni ya kwanza kwa bandari kubwa zaidi nchini kupata tuzo katika kipengele cha crème de la crème kilichojumuisha bandari nyingine kama Bandari za Elizabeth, Cape Town na Durban zote za Afrika Kusini, Bandari ya Mobasa, Kenya na Bandari ya Zanzibar.
Mwandishi Diramakini anaendelea kukusanyia data zaidi kwa ajili ya kukujuza kuhusiana na rasilimali za Tanzania zilivyo na matokeo chanya ndani na nje ya Tanzania, hivyo endelea kufuatilia hapa.