Bunge lawaita wabunge wote wateule bungeni Dodoma

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Stephen Kagaiga ametangaza kuanza kwa Bunge la 12 Novemba 10, mwaka huu jijini Dodoma, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Pia kupitia taarifa aliyoitoa leo Novemba 7, 2020 amewataka wabunge wote wateuliwa kufika katika ofisi za Bunge wakiwa na nyaraka mbalimbali kwa ajili ya kujisajili.

 

Stephen Kagaiga amesema, usajili wa wabunge unaanza leo Novemba 7 hadi 9, 2020 katika ofisi za Bunge jijini Dodoma. Miongoni mwa nyaraka wanazopaswa kufika nazo ni pamoja na hati ya kuchaguliwa au kuteuliwa,nakala ya kitambulisho cha Taifa cha NIDA, kadi ya benki ya Mbunge  na cheti  cha ndoa kinachotambuliwa na Serikali.

Amezitaja nyaraka nyingine kuwa ni vyeti vya kuzaliwa vya watoto walio chini ya umri wa miaka 18 ,vyeti vya elimu ya Mbunge ambavyo husaidia namna ya kuwapanga wabunge katika kamati za Bunge pamoja na picha ndogo nane.

Katibu huyo amesema, shughuli zitakazofanyika katika mkutano huo ni pamoja na kusomwa kwa tangazo la Rais la kuitisha Bunge, uchaguzi wa Spika, kiapo cha uaminifu kwa wabunge wote, kuthibitisha jina la Waziri Mkuu,ufunguzi rasmi wa Bunge jipya utakaofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Poimbe Joseph Magufuli.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news