Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt.Bashiru Ali amesema, chama kimeongeza muda wa uchukuaji fomu za kuwania Uspika, Unaibu Spika, Wenyeviti wa Halmashauri na Mameya wa Manispaa na Majiji nchini, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Dkt.Bashiru Ali ameyasema hayo leo Novemba 3,2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.
Katibu Mkuu huyo amesema, kwa nafasi ya Uspika fomu zitaendelea kutolewa na kurejeshwa hadi kesho Novemba 4,200 saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Kwa upande wa Wenyeviti na Mameya Dkt. Bashiru amesema, mwisho utakuwa Novemba 5,2020 ili kupanua demokrasia na kupata fursa ya kuchambua na kuongeza ufanisi wa usimamizi wa fedha na mali za umma.
Pia amesema, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM itafanya kikao chake Novemba 6, mwaka huu jijini Dodoma kwa ajili ya kupitisha majina ya walioomba Uspika wa Bunge na kupokea taarifa ya awali ya utekelezaji wa mpango wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. Uchaguzi ambao ulifanyika Oktoba 27 na 28, mwaka huu.
Tags
Habari