|
"Kamati Kuu imewavua dada zetu hawa nyadhifa zote za uongozi na mamlaka ndani ya chama, kamati kuu imeona wamepoteza sifa;anaripoti Mwandishi Diramakini.
| | | |
|
Hayo yamebainishwa leo Novemba 27, 2020 na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.
Mbowe aliyasema hayo usiku huu wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amesisitiza kuwa, chama hicho hakikuteua wabunge wa viti maalum.
Wabunge hao ni Halima Mdee,Asia
Mohamed, Felista Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti
Majala, Stella Simon, Anatropia Theonest,Salome Makamba, Conchester
Lwamraza, Grace Tendega, Ester Matiko,Secilia Pareso,Ester Bulaya, Agnes
Kaiza, Nusrat Hanje, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga na Tunza Malapo.
Novemba 24,2020 Mbunge wa Viti
Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Bi. Halima Mdee
aLIwaahidi wanachama wa chama hicho kuwa wanakwenda bungeni kufanya kazi
kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.
Mdee aliyasema hayo katika viwanja vya Bunge leo muda mfupi baada ya kula kiapo pamoja na wabunge wenzake 18.
Mbunge
huyo ambaye awali alikuwa Mbunge wa Kawe na ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) aLImshukuru Mheshimiwa Spika,
Job Ndugai kwa kusimamia kiapo chao.
"Mheshimiwa
Spika nikushukuru kwa kiapo kufanyika na kukamilika, nikishukuru chama
changu kupitia wao sisi tumepata nafasi hii ya kukiwakilisha chama
chetu. Viti hivi sio hisani ni sehemu ndogo ya ushindi mkubwa ambao
chama chetu kilipata.
"Nikuhakikishie
Mheshimiwa Spika tutafanya kazi kwa uaminifu kama kambi rasmi ya
upinzani bungeni na kwa uadilifu mkubwa kwa viwango vilevile tulivyokuwa
tunavifanya. Kuna vijana wapya sisi kama dada zao tunakuhakikishia
watafanya kazi bora. Niwahakikishie wana CHADEMA tutafanya kazi
mliyotutuma kwa uaminifu na uadilifu mkubwa sana,"amesema.
Freeman Mbowe ameongeza kuwa, Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi leo Novemba 27,2020 imeazimia kuwavua uanachama wanachama na viongozi hao.
"Wamekinajisi chama na wamekataa kuja kwenye Kamati Kuu. Chama chetu hakijateua wabunge wa Viti Maalum tunaona tu watu wetu wanaapishwa na hatuna taarifa, hatujapeleka majina, fomu za tume zipo ofisini, mama zetu hawa, dada zetu hawajajaza fomu, ila tunaona tu wanaapishwa. Kamati Kuu imewavua uongozi wale wote ambao walikuwa viongozi kwenye mabaraza kati ya hao dada zetu 19 sitaki kupoteza muda kuwataja majina, kwa hiyo kuanzia sasa hawapaswi kushughulika na lolote kama viongozi na tumeelekeza nafasi zao zizibwe haraka,"amefafanua Freeman Mbowe.