Diamond kurudiana na Zari? Siri yaanikwa

 Chanzo cha karibu kimemudokeza Mwandishi Diramakini kuwa, jambo usilolijua ni kama usiku wa giza kwani, huenda uhusiano wa wapenzi maarufu Afrika Mashariki yaani msanii wa bongo fleva Diamond Platinumz na mfanyabiashara wa Uganda Zari Hassan ukarejea.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, siku moja baada ya Zari Hassan kumletea Diamond watoto wake jijini Dar es Salaam, imeonekana kuna viashiria vya wazi kuwa, wawili hao bado upendo wao ni wa kudumu na hakuna pingamizi.

Hatua hiyo inakuja baada ya mwaka 2018 wawili hao kuonekana kutofautiana, hivyo Zari kutangaza kuachana na mzazi mwenzake, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platinumz baada ya kuwapo kwa tuhuma nyingi kuhusu mwanamuziki huyo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengine. Endelea kufuatilia hapa, Mwandishi Diramakini anakuandalia ripoti kamili...

Mahusiano ya wawili hawa Diamond na Zari yaliungwa mkono na mamilioni ya wana Afrika Mashariki baada ya kuonekana kuwa ni kati ya pendo lenye tija na tabasamu kubwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news