Diwani Mteule Kata ya Kikongo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini mkoani Pwani, Fatuma Ngozi na wajukuu zake wawili wamekufa baada ya nyumba yake kuchomwa moto usiku wa kuamkia leo Novemba 9, 2020, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Ngozi ni miongoni mwa madiwani wateule kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliopata ushindi wa kishindo baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28,2020.
Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa.
Amesema, uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo cha moto huo ambao umesababisha vifo hivyo na kubaini ukweli unaendelea na taarifa kamili itatoka muda wowote.
Pia amesema, maiti zimehifadhiwa katika Hospitali Mlandizi wakati wakiendelea na uchunguzi na baada ya hapo watakabidhi kwa ndugu kwa ajili ya shughuli za maziko.
Amesema, kwa upande wa majeruhi waliokolewa kwenye nyumba hiyo wanaendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha mkoani Pwani.
Tags
Habari