Dkt.Jumma Mhina atoa rai kwa vyama, wanasiasa wilayani Longido

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido, Dkt.Jumma Mhina amevitaka vyama vya siasa pamoja na wagombea wao walioshiriki katika uchaguzi Mkuu wa jimboni hilo kumuunga mkono Mbunge mteule wa jimbo hilo, Steven Lemomo ili aweze kutekeleza mipango ya maendeleo aliyonayo kupitia chama chake na halmashauri hiyo, anaripoti Pamela Mollel (Diramakini), Longido.
Ameyasema hayo wakati akitangaza matokeo ya uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Longido ambapo alimtangaza Dkt.Lemomo kuwa mshindi halali wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Dkt.Mhina amesema kuwa, vyama vya siasa katika jimbo hilo kuwa kitu kimoja kwa kuwa uchaguzi umekwisha na Mbunge aliyepita ni wananchi wote atakayewaletea maendeleo.

"Ndugu wananchi baada ya uchaguzi kuna maisha, sisi ni ndugu,sisi ni marafiki,sisi ni jamii moja tudumishe amani tuliyonayo,"amesema Dkt.Mhina. Aidha, alisisitiza suala la amani kama ambavyo Rais John Pombe Magufuli aliwasisitizia Watanzania wote.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe amesema kuwa, Serikali haitasita kumchukulia hatua mtu ambaye atahamasisha au atashiriki kuwa miongoni wataakaoanzisha vurugu au maandamano.

Mwaisumbe amesema kuwa, maandamano hayo hayapo kisheria hivyo mtu au kikundi watachukuliwa hatua kali na Serikali haitafumbia macho jambo hilo.Aidha, amesema kuwa wanaofanya hivyo ni kutaka madaraka yasiyo halali.

"Tunazo tetesi kwa baadhi ya viongozi walioshindwa katika uchaguzi wameamua kuitisha maandamano ya kuleta vurugu na kuvunja amani tuliyonayo,"amesema Mwaisumbe.

Vyama vya siasa vilivyoshiriki katika Uchaguzi Mkuu nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo CCM, Steven Lemomo kura 61,885 , CHADEMA,Lukas Laizer kura 1,037 ,Kombo Mkadam wa CUF kura 65,Juma Feruziyson wa NRA kura 21. Idadi ya wapiga kura walioandikishwa katika jimbo hilo ni 76,814,waliopiga kura 63,465,idadi halisi waliopiga kura 63,008,kura zilizokataliwa ni 457.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news