Siku chache baada ya Mgodi wa Kuchimba Dhahabu wa Geita (GGML) kutoa shilingi milioni 800 kwa ajili ya kujenga Kijiji cha Maonyesho na Kituo cha Uwekezaji Ukanda Maalum wa Kiuchumi (EPZA) na milioni 50 kwa ajili ya kutengeneza magari ya kutumia umeme,sasa mgodi huo umetoa milioni 70 kwa ajili ya kujenga bustani ya kisasa katikati ya mji wa Geita, anaripoti Robert Kalokola (Diramakini),Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akimuonyesha mchoro wa Bustani ya kisasa Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Richard Jordinson mwingine ni Meneja Mahusiano wa GGML, Joseph Mangilima. (DIRAMAKINI).
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akizindua ujenzi wa Bustani hiyo kwa kushiriki kuchimba msingi amesema, mgodi huo umekuwa na ushirikiano mkubwa na Serikali katika shughuli za maendeleo kwa kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo katika mkoa huo.
Amesema, katika Halmashauri ya Mji wa Geita limetengwa eneo maalum ambalo ni Ukanda Safi kwa ajili ya kujenga Bustani (Smart Area) ambalo amesema litaanzia kwenye mlango wa kuingia mgodi wa GGML hadi Hoteli ya Lenny eneo la Bombambili Mjini Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel ameongeza kuwa, Halmashauri ya mji wa Geita imeamua kujenga Bustani ya kisasa katikati ya mji huo ili wananchi wawe wanapata eneo la kupumzikia hasa baada ya kazi.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert, Mkurugenzi mtendaji wa GGML Richard Jordinson na Meneja Mahusiano wa GGML Joseph Mangilima wakiteta jambo baada ya uzinduzi wa ujenzi wa Bustani ya kisasa katikati ya mji wa Geita.(DIRAMAKINI).
Ameyataka makampuni mengine ambayo yana mikataba ya kutoa huduma ndani ya Mgodi wa GGML kuhakikisha yanashiriki katika kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo katika mkoa kama mgodi huo unavyoshiriki shughuli hizo kwa kuchangia fedha za miradi.
Afisa Mipango wa Halmashauri ya mji wa Geita, Malima Magesa amesema, mradi huo wa ustani umepangwa kutumia milioni 70 kutokana na fedha za huduma kwa wananchi (CSR) zinazotolewa na mgodi wa GGML.
Malima Magesa ambaye pia ni Mwenyekiti wa CSR ameongeza kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya mwezi mmoja kuanzia Sasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Richard Jordinson akizungumza katika uzinduzi huo amesema kuwa, mgodi huo unafurahi kushirikiana na jamii na kuwa sehemu yake hasa katika kusaidia katika shughuli za maendeleo yao.
Amesema, GGML imetenga fedha hizo milioni 70 kwa ajili ya kujenga Bustani hiyo na kwamba anaamini mradi huo utatekelezwa kama ulivyopangwa.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel (mwenye sululu) akichimba msingi katika uzinduzi wa ujenzi wa Bustani ya kisasa katikati ya mji wa Geita inayotarajiwa kutumia sh. milioni 70 kutoka GGML. (DIRAMAKINI).
Mradi huo wa Bustani ya kisasa ni moja ya miradi mingi ambayo inatarajiwa kutekelezwa katika mpango wa CSR wa mwaka 2020/2021 katika Halmashauri ya mji wa Geita.
Richard Jordinson ameongeza kuwa, mgodi huo utaendelea kushirikiana na jamii ya Geita katika shughuli mbalimbali kwa manufaa ya jamii nzima ya Geita na jamii inayowazunguka.
Mgodi wa GGML utenga jumla ya sh.Bilioni 9.2 kwa mwaka 2020/ 2021 za Mpango wa Uwajibikaji kwa jamii (CSR) ambapo umesaini makubaliano na Halmashauri mbili ya Geita Mji pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Geita ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika jamii.