Winga wa Real Madrid, Eden Hazard amefunga bao lake la kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kujiunga na timu hiyo akitokea Klabu ya Chelsea siku za karibuni, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Katika mtanange huo uliopigwa uwanja wa San Siro, Hazard amefunga bao hilo kwa mkwaju wa penalti dakika ya saba huku lile la pili likiwa ni la kujifunga kutoka kwa mchezaji wa Inter Milan, Achraf Hakimi dakika ya 59.
Aidha, Klabu ya Inter Milan ilikubali kufungwa mabao 2-0 ikiwa nyumbani katika uwanja huo na kuifanya ipoteze jumla ya mechi mbili na kuwa na sare mbili kati ya mechi nne ilizocheza ndani ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika msimamo wa kundi B, klabu hiyo ipo nafasi ya nne na Real Madrid wao wapo nafasi ya pili na alama zao wakiwa wamejikusanyia saba.
Hazard aongoza ushindi wa Real Madrid
Tags
Michezo