Ilemela watoa tamko la pongezi kwa Rais Magufuli, Mabula, madiwani

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza kwa pamoja wametoa tamko la kumpongeza aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Urais kupitia chama hicho, Rais Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, mgombea ubunge Dkt.Angeline Mabula, madiwani wote 19 wa kata za jimbo hilo na wale wateule kupitia viti maalum kwa ushindi mkubwa na wa kishindo, anaripoti Mwandishi Diramakini

Pongezi hizo zimetolewa Novemba 27, 2020 wakati wa kikao maalum cha halmashauri kuu ya wilaya hiyo kilichoongozwa na Mwenyekiti wake, Nelson Mesha kikiwa na lengo la kutathimini namna zoezi zima la uchaguzi lilivyoendeshwa ndani ya wilaya hiyo ambapo kwa pamoja wakakubaliana kuridhishwa na jitihada na mchango wa kila mwanachama katika kukipatia ushindi chama hicho.


Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Dkt.Angeline Mabula. (Diramakini).

Sambamba na kukubaliana kuwapongeza wagombea wote wa chama chao kwa ushindi wa nafasi mbalimbali za uchaguzi uliofanyika nchini Oktoba 28, 2020 ambapo katika wilaya hiyo mgombea wa nafasi ya Urais alipata ushindi kwa asilimia 91 na mbunge alishinda kwa asilimia 84 huku kata zote 19 zikichukuliwa na wagombea wa Chama Cha Mapinduzi. 

"Wakati wenzetu wakiendelea kulalamika duniani sisi tunajipanga kuchapa kazi, CCM wilaya ya Ilemela leo tunatoa tamko rasmi la kumpongeza Rais Dkt.John Magufuli, Mbunge Dkt.Angeline Mabula na madiwani wa kata zote kwa ushindi wakiwemo na wale wa viti maalum,"amesema Mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela, Bi Aziza Isimbula amewatakia heri ya utekelezaji mwema wa Ilani ya uchaguzi wagombea hao walioshinda nafasi mbalimbali za uchaguzi huku akisisitiza kuwa ushindi huo unaashiria kuwa na Ilemela ya Kijani

Akihitimisha mbunge wa jimbo la Ilemela, Dkt.Angeline Mabula mbali na kuwashukuru wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na wananchi kwa ujumla kwa kukiamini chama chake na kuwapigia kura za ushindi wagombea wote wa chama hicho akaahidi kufanya ziara kwa wanachama na wananchi katika maeneo yao wanayoishi ili kusikiliza ushauri, kero na changamoto zinazowakabili na kisha kuzipatia ufumbuzi.
 
Pia ameipongeza Kata ya Kahama kwa kitendo cha wananchi wake kuongoza katika kujitokeza kupiga kura kwa zaidi ya asilimia 99.3, Kata ya Mecco kwa kuwa ya pili kwa asilimia 91 na ya tatu ikiwa Kayenze.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news