Jezi za Yanga, Simba SC kutolewa bure MOI leo

Kuelekea mechi ya watani wa jadi kati ya timu ya mpiga wa miguu ya Simba SC na Yanga SC Novemba 7, 2020, Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa kushirikiana na mfanyabiashara Azim Dewj na wadhamini wa Yanga, GSM pamoja na Ramarid Sport wa Simba leo Novemba 6, 2020 inaendesha kambi ya uchangiaji damu ambapo wachangiaji watazawadiwa jezi za timu wanazoshabikia, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano katika Taasisi ya MOI, Patrick Mvungi kupitia taarifa aliyoitoa kwa umma.

Amesema, kambi hiyo ya uchangia damu inalenga kutatua changamoto ya upatikanaji wa damu katika Taasisi ya MOI ambapo kambi inafanyika leo Ijumaa Novemba 6, 2020 kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika eneo la maegesho ya magari katika Kitengo cha MOI cha zamani.

"Damu itakayokusanywa itatumika kuokoa maisha ya majeruhi wa ajali, watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi na wagonjwa wenye uhitaji wa kuongezewa damu. Hivyo, Taasisi ya MOI inawakaribisha mashabiki wa timu ya Simba na Yanga pamoja na wadau wengine kujitokeza kwa wingi leo Ijumaa kuchangia damu. Changia damu, okoa maisha,"ameeleza Mvungi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news