Joe Biden, Kamala wajiandaa kwenda White House

Mgomba urais wa Chama cha Democratic nchini Marekani, Joe Biden amesema anatarajia kushinda uchaguzi mkuu wa Marekani.

Hayo yanajiri ikiwa Makamu huyo wa zamani wa Rais anaonekana kumuacha mbali Rais aliyepo madarakani na mgombea urais, Donald Trump ingawa Trump ameendelea na msimamo wake wa kutokubali kushindwa na ameshachukua hatua zaidi.
Licha ya ujasiri huo wa Biden, vyombo vya habari vimeamua kuwa kimya kuepuka kujiingiza katika mtego wa kukurupuka kutangaza kuwa, Joe Biden ameshinda ingawa matokeo yanaonyesha wazi wazi huku kura zikiendelea kuhesabiwa kuwa, ushindi wake umekaribia.

Wakati akizungumza Novemba 6, 2020, Joe Biden amesema kura ambazo zimeshahesabiwa ni ushahidi tosha kuwa atashinda hivyo yeye na mgombea mwenza Kamala Harris wameanza kukutana na wataalumu kuandaa safari ya kuingia Ikulu ya Marekani ya White House.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news