LIVE:Uapisho wa Mwanasheria Mkuu Tanzania, Prof. Adelardius Lubango Kilangi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alimteua, Prof. Adelardius Lubango Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Novemba 5,2020 na leo anaapishwa katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

“Pamekuwa na tabia kila Serikali mpya inapoingia watu wanakuwa na hofu hasa watendaji ndani ya Serikali kwamba panatokea mabadiliko na kwa sasa wakuu wa mikoa na wilaya naona wanakuwa na hofu na nawashangaa kwa nini wanapata hofu maana kama mafanikio ya Serikali ni pamoja nao.

"Kama ushindi wangu wa asilimia 84.4 umechangiwa pia na wao kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa miaka mitano, wasiwasi wa nini?, Naona meseji za baadhi ooh mheshimiwa mimi nimefanya kazi sana.

“Narudia watendaji wa Serikali wachape kazi wasiwe na wasiwasi, hakuna mabadiliko tulianza wote tunamaliza wote, yaani nianze kuapisha tena wakuu wa mikoa 26 siwezi, hata kuapisha kunachosha, watu wachape kazi waliokuwepo watabaki walewale labda watakaostaafu au kuwa na utendaji mbovu,"amefafanua Rais Dkt.John Pombe Joseph Magufuli leo Novemba 9,2020.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news