Maandamano ya CHADEMA, ACT Wazalendo yasusiwa

Wananchi mkoani Njombe wakiwemo wajasiriamali na wafanyabiashara wa Halmashauri ya Mji wa Njombe mkoani humo wamepinga vikali madai ya baadhi ya wanasiasa kuhamasisha maandamano kwa ajili ya kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi huku wakitoa wito kwa watanzania kuendelea na shughuli zao za kujitafutia kipato.

Hayo wameyabainisha ikiwa ni siku moja baada ya viongozi wa vyama vya ACT Wazalendo na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushinikiza maandamano ambayo hata hivyo yameonekana kususwa nchi nzima, kwa mujibu wa wawakilishi wa Diramakini mikoani wamesema kila mwananchi alikuwa busy na kazi zake.

Makundi hayo ya wananchi mjini Njombe wamesema wanaamini uchaguzi umekwisha hivyo ni rai yao kwa sasa kujikita na uzalishaji ili kuinua vipato vyao kuliko kuingia barabarani.

Philimon Edward ni mwenyekiti wa bodaboda Mkoa wa Njombe amesema, hawezi kushauri na hayuko tayari kuruhusu dereva bodaboda yeyote kuingia barabarani kwa kuwa nia yao ni maendeleo.

"Sitashauri na siko tayari kuruhusu dereva bodaboda yeyote aingie kwenye maandamano, sisi nia yetu ni maendeleo, amani na watanzania wajue sisi tunafanya kazi hii kama kazi nyingine kwa sababu ukiingia kwenye maandamano maana yake umesahau wajibu wako,"amesema Mwenyekiti huyo.

"Hakuna mtu aliyelazimisha kupiga kura na kila mmoja alikuwa na uhuru, lakini kulikuwa na malalamiko kwa baadhi ya vyama vya upinzani. Mimi niombe taratibu za kuandamana si sawa kwa kuwa nchi yetu imeunda sheria kinachotakiwa ni kufuata sheria na kufuata utaratibu kwenye ofisi zinasohusika kwa mijadala kama unaona haki haikutendeka, lakini si maandamano na ukiangalia Njombe kumekuwa na utulivu wa kipekee kuliko miaka mingine kwa kweli watu walitulia mno,"amesema.

Kwa upande wake, Daniel Kidenya ambaye ni mjasiriamali wa stendi ya zamani ya mji wa Njombe anasema, matokeo yaliyoptaikana kwa Chama Cha Mapinduzi walikuwa na uhakika nayo kutokana na namna walivyotekeleza ilani yake mwaka 2015-2020.

"Binafsi matokeo nilikuwa na uhakika nayo kwa Magufuli (Rais Dkt.John Magufuli) kutokana na baadhi ya vitu kwenye Ilani yao vilivyotekelezwa na pia sisi wananchi wa ngazi ya nchini tumeweza kunufaika kwenye utafutaji wetu,tutulie sasa tufanye kazi kwa kuwa uchaguzi umeisha na tuendelee kumunga mkono Rais katika harakati zake ili tutoke kwenye uchumi wa kati na kuingia kwenye uchumi wa juu,"amesema Mjasiriamali huyo.
Kwa upande wake,Patrick Mgaya ambaye ni mwalimu mstaafu ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu kwa kuwa demokrasia imetumika huku akiwataka wasioridhika kudai haki zao kwa kufuata taratibu za kisheria.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news