Magonjwa yasiyoambukiza kwa mwaka 2017 yalichangia vifo kwa asilimia 33-Makubi

Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Abel Makubi amesema kuwa takwimu za kitaifa zinaonesha asilimia 33 ya vifo vyote nchini Tanzania vimetokana na magonjwa yasiyoambukiza kwa mwaka 2017, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kauli hiyo ameitoa mapema jijini Dar es Salaam wakati alipokua akifungua kongamano la pili la kisayansi la maadhimisho ya wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza ambapo amesema kuwa jumla ya vifo 134, 600 viliripotiwa na kuhusishwa na magonjwa yasiyoambukiza. 

"Vifo hivyo vimetokana zaidi na magonjwa ya moyo na shinikizo la damu kwa asilimia 13, kisukari asilimia mbili, saratani asilimia saba na ajali asilimja 11, hali hii kwa ujumla haikubaliki na inatufanya tuhjumuike katika kujitathmini na kupanga mikakati ya pamoja ili tukubalike na changamoto hii," amesema Prof.Makubi. 

Aidha amesema, hali hiyo haikubaliki hivyo wanapanga mikakati ya pamoja ili kukabiliana na changamoto hiyo ambayo inaongeza utegemezi sugu kwa familia na kuongeza mzigo mkubwa kwenye mfumo wa afya kwa kuwa ni magonjwa ya muda mrefu na yanatumia rasilimali nyingi.

Hata hivyo amesema kupitia Kongamano hilo Serikali inatarajia kupata mapendekezo ya wadau wa Afya ili kuweza kuimarisha huduma za kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukiza hivyo ni vyema yawe mapendekezo ya kutekelezeka.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya Dkt.Grace Magembe amesema kwa takribani miaka nane magonjwa yasiyoyakuambukiza yamekuwa yakiongezeka ikiwa ni pamoja na gharama za matibabu.

Aidha ameongeza kuwa lengo la Kongamano hilo ni kutoa uelewa kwa jamii kuhusu magonjwa hayo na njia za kukabiliana nayo ambapo katika wiki ya maadhimisho watatoa elimu kupitia sehemu mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari pamoja na kutoa huduma ya upimaji katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. 

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa magonjwa yasiyoyakuambukiza yanachangia zaidi ya vifo milioni 41 ambayo ni sawa na asilimia 71 ya vifo vyote milioni 57 vilivyotokea mwaka 2016 huku mataifa ya Uchumi wa kati na chini kama Tanzania yakionekana kuathirika zaidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news