Makachero Kenya wamnasa Godbless Lema, mkewe na watoto wakitoroka

Maafisa Usalama nchini Kenya wanamshikilia aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema akiwa na mkewe na watoto wakijaribu kutoroka nchini, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Lema amekamatwa na Polisi katika Kaunti ya Kajiado nchini Kenya baada ya yeye na familia yake kuvuka mpaka wa Namanga akieleza kuwa, anakwenda kutafuta hifadhi katika Ubalozi wa Marekani nchini humo.

Kwa mujibu wa Afisa mmoja kutoka mjini humo ameidokeza Diramakini kuwa, Lema na familia yake wanakabiliwa na makosa makubwa ya kuvuka mpaka bila nyaraka muhimu. 

Afisa huyo amesema, maafisa wa Uhamiaji walikataa kugonga muhuri nyaraka zilizowasilishwa na mke wa Lema, Neema Godbless Lema kwa madai hadi wamuone Godbless Lema mwenyewe.

Aidha, Lema alikwenda, akawaambia hana hati yake ya kusafiria kwa sababu alikuwa hasafiri, bali watoto wake walikuwa wanakwenda kutafuta shule, dai ambalo linatajwa lilikuwa halina ukweli.

Hata hivyo,maafisa waliruhusu mke na watoto kuvuka mpaka huku Godbless Lema akiomba kwenda kutafuta fedha za Kenya ili ampe mke wake kwa ajili ya matumizi na taratibu zingine

Afisa huyo amesema, Lema alipovuka mpaka na familia yake walingia ndani ya gari la Mwanasheria wake, George Luchiri huku akijua wazi kuwa amedanganya tangu awali.

Kwa mujibu wa Gorge Luchiri amesema, alitaka ampeleke Lema,Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UNHRC) mara tu atakapavuka mpaka huo.

Wakati huo huo, Afisa mmoja mwenye cheo cha juu nchini Kenya amesema,Godbless Lema atarudishwa Novemba 9, 2020 nchini Tanzania baada ya kwenda nchini humo kutafuta hifadhi kwa UNHRC ingawa chanzo kingine kinasema lengo lilikuwa kupata hifadhi Ubalozi wa Marekani nchini humo.

Godbless Lema anashikiliwa Kituo cha Polisi cha Kajiado huku akidai maisha yake yapo hatarini, jambo ambalo limetajwa na wachambuzi wa masuala ya usalama kuwa, dhamira yake huenda ni mkakati wa chama kutafuta huruma kwa jumuiya ya Kimataifa ili kuipaka Tanzania matope.

"Kwa maana nyingine tunaweza kusema hizi ni siasa za kitoto, tena sana. Na hii tabia isipokomeshwa kwa watu wenye maono mafupi namna hii kama Mheshimiwa sana, Lema naona anguko baya zaidi la CHADEMA huu si mwenendo mzuri na hauna afya kwa chama. Lema ni nani hadi adai kuwa anatishiwa usalama wake," Mchambuzi amemdokeza Mwandishi Diramakini, ripoti hii inaendelea hapa...

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news