Joe Biden ashinda Urais Marekani

Mgombea Urais wa Chama cha Democratic nchini Marekani Joe Biden ameshinda uchaguzi wa Marekani na kuwa rais mteule wa Marekani baada ya kumshinda Donald Trump, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Joe Biden ameshinda katika jimbo muhimu la Pennsylvania, akijizolea kura zaidi ya 270 zilizohitajika ili kuchukua kiti cha White House.
Kampeni ya Donald Trump imeonesha mgombea wao hana mpango wa kukubali matokeo ya uchaguzi huo. Matokeo hayo yanamfanya Trump kuwa rais wa kwanza kutumikia awamu moja madarakani tangu miaka ya 1990.

Uchaguzi huu umeshuhudia watu wengi wakijitokeza kupiga kura tangu miaka ya 1900. Aidha, Joe Biden ameshinda zaidi ya kura milioni 73 mpaka sasa, idadi ya juu kuwahi kutokea kwa mgombea yoyote yule Marekani. Trump akipata kura zaidi ya milioni 70 akishika nafasi ya pili kwa idadi kubwa katika historia ya Marekani.

Rais Trump alijitangaza mshindi wa uchaguzi wakati kura zikiendelea kuhesabiwa. Wakati wote amedai kuwa zoezi la kuhesabu kura limekuwa na dosari, lakini hajawasilisha ushahidi wowote kuhusu madai yake.

Timu ya kampeni imefungua kesi katika majimbo mbalimbali mapema Ijumaa, wakati Joe Biden alipokuwa akikaribia kunyakua ushindi huku akisisitiza uchaguzi huu haujaisha. Kwa matokeo hayo, Joe Biden anakuwa Rais wa 46 wa Marekani

Joe Biden ni nani?

Joseph Robinette Biden Jr (Joe Biden) ni mwanasiasa wa Marekani ambaye alihudumu nafasi ya 47 ya Makamu wa Rais nchini Marekani chini ya utawala wa Rais Barack Obama kuanzia 2009 Hadi 2017. Ni mwanachama hai wa Chama cha Democratic ambaye kabla alikuwa Seneta wa Jimbo la Delaware kuanzia 1973 hadi 2009.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news