Akitangaza matokeo hayo leo Jumamosi, Novemba 21, 2020 jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Charles Msonde amesema watahiniwa waliofutiwa mitihani hawatapata nafasi nyingine ya kurudia mitihani hiyo, anripoti Mwandishi Diramakini
.Dkt.Msonde amesema, pamoja na Kamati ya Mitihani kutimiza wajibu wao vizuri, kulijitokeza matukio machache ya udanganyifu wa mitihani katika baadhi ya shule nchini.
.Dkt.Msonde amesema, pamoja na Kamati ya Mitihani kutimiza wajibu wao vizuri, kulijitokeza matukio machache ya udanganyifu wa mitihani katika baadhi ya shule nchini.
"Jumla ya shule 38 sawa na asilimia 0.22 ya shule zote za msingi 17,329 zilizofanya mitihani, zimebainika kufanya udanganyifu wa mitihani kwa namna mbalimbali. Watahiniwa 1,059 sawa na asilimia 0.1 ya wote 1,023,950 waliofanya mitihani walibainika kudanganya,” amesema Dkt. Msonde.
BONYEZA MKOA HUSIKA HAPA CHINI UWEZE KUJISOMEA MATOKEO
|
Amesema, shule hizo zilifanya makosa mbalimbali ikiwemo kuiba mitihani, kugawa majibu kwa wanafunzi na kubadilisha watahiniwa kwa kuwaweka wasio halisi kuwafanyia mitihani wanafunzi watoto.
Tags
Habari