Miili 17 yagundulika katika makaburi ya pamoja

Zaidi ya miili ya watu 17 imegunduliwa katika makaburi ya pamoja mkoani Tarhuna uliopo Magharibi mwa Libya,anaripotri Mwandishi Diramakini.

Mkuu wa Kikosi Kazi cha Umoja wa Mataifa ambacho kina jukumu la kuwatafuta watu ambao wamepotea,Lotfi Tawfiq amesema,miili hiyo imebainika Alhamisi ya wiki hii, baada ya kufukuliwa makaburi matano tofauti.

Sehemu ya makaburi kwa mujibu wa mamlaka nchini Libya. [REUTERS].

Tawfiq amesema, makaburi hayo yapo eneo la Tarhuna eneo ambalo mbabe wa kivita Khalifa Haftar alianzisha mashambulizi yake kuelekea mjini Tripoli ambapo ndipo ilipo Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayotambulika na Umoja wa Mataifa.

Eneo hilo ambalo lipo zaidi ya kilomita 80 kutoka mjini Tripoli ni mara ya kwanza kugundulika idadi hiyo kubwa tangu mbabe huyo ajiondoe mwezi Juni.

Waziri wa Mambo ya Ndani kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNA), Fathi Bashagha amesema, makaburi hayo yanabeba ujumbe wa ishara mbaya ambayo haikubaliki katika jamii.

Bashagha amesema, miongoni mwa miili hiyo mmoja ni wa Mabrouk Khalaf ambaye alikuwa Mkuu wa Mawasiliano ambapo, idadi hiyo inafanya jumla ya miili iliyofukuliwa katika miezi ya hivi karibuni ku.fikia 112 nchini humo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news