Mkurugenzi Sheilla Lukuba ahamasisha usafi wa mazingira Morogoro

Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro mkoani Morogoro Sheilla Lukuba amewataka wananchi wa Manispaa ya Morogoro kuyatunza mazingira kwa kufanya usafi na kuhifadhi taka maeneo husika.

Lukuba amesema kila mwananchi ana jukumu la kufanya usafi katika mazingira anayoishi wa kuhakikisha yanakuwa safi muda wote kwa lengo la kuepuka maradhi yakiwemo kipindupindu,kichocho na malaria.


"Naomba wananchi watambue na kuamini kuwa usafi ni tabia , hivyo tunatakiwa kuweka safi mazingira yetu na yale wanayoishi watu wenye mahitaji maalum ili nao waishi kwa amani, utulivu na usalama wa afya zao kama wanavyoishi watu wengine,"amesema Lukuba.

“Lakini bado tuna barabara zetu wengine sio wastaarabu wanatupa taka hovyo kwenye mitaro , niwaombe tuanze kutunza mitaro yetu, ikiziba ni hatari sana kwani inaponyesha mvua mitaro ina jaa na maji yanashindwa kufuata mkondo na kusababisha mafuriko ,"ameongeza Lukuba.

Aidha, amewaagiza Maafisa Afya wa kata na mitaa kuwajibika kuwasimamia wananchi kuyasafisha maeneo yao na kutunza mitaro inayopita maeneo yao,"amesema Lukuba.

Ameongeza kuwa, lengo la Manispaa hiyo ni kufika kiwango cha kutajwa katika Miji misafi, Kitaifa, Kikanda na Kitaifa kama inavyotajwa miji mingine ikiwamo Moshi, Arusha na Iringa.

Mwisho, amewataka wananchi kujenga tabia ya kufanya usafi kwa hiari ili kuondokana na magonjwa yanayoweza kuzuilika.

Maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira Dunianiani yameaanza leo tarehe 16/11/2020 na yatafikia tamati yake tarehe 19/11/2020. Maadhimisho haya yanaambatana na kauli mbiu isemayo“Zingatia mahitaji ya jinsia kwa usafi wa mazingira endelevu”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news