Mo Dewji ataja dhuluma ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Soka ya Simba, Mohammed Dewji amedai kamwe mpira wa Tanzania hautasonga mbele kutokana na mwenendo wa uchezeshaji uliopo, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mo Dewji ametoa malalamiko hayo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, akitolea mfano goli la Luis Miquissone dhidi ya Mwadui FC, lililokataliwa kwa madai kuwa ni la kuotea. 

"Bado dhulma juu yetu inaendelea. Kwa mwenendo huu, mpira wetu hapa Tanzania kamwe hauwezi kusonga mbele,"ameeleza Mo Dweji.

Waamuzi wa Tanzania wamekuwa wakilalamikiwa juu ya uchezaji wao hususani kwenye maamuzi yenye utata kama ya kuotea na matukio ya katikati ya uwanja.

Hivi karibuni Shirikisho la soka Tanzania kupitia Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Soka Tanzania bara ilimfungia mwamuzi Shomari Lawi miezi 12 kutojihusisha na soka kutokana na makosa mbalimbali katika kazi yake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news