Mvua kubwa yaua, yajeruhi wanafunzi

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limethibitisha vifo vya watu wawili na wengine watatu kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi wakati mvua kubwa ikinyesha mkoani humo, anaripoti Mwandishi Diramakini.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama amesema leo Novemba 9, 2020 kuwa, tukio hilo lilitokea Novemba 8, mwaka huu, majira ya saa tano asubuhi wakati mvua hiyo ikinyesha huku ikiambatana na radi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani humo.

Manyama amewataja marehemu kuwa ni Khalifan Yassin (18) mkazi wa Gezaulole Kata ya Gungu mbaye alipigwa na radi na kupoteza maisha katika eneo ambalo alikuwa amejikinga na mvua.

Sambamba na mwili wa mtu anayedhaniwa kuwa na umri wa miaka 10 ambaye hajafahamika hadi sasa ambaye alisombwa na maji na mwili wake kuokotwa kandokando ya mto Kata ya Kibirizi.

Kamanda Manyama amesema, mvua hiyo iliyokuwa inayesha ikiambatana na radi mbali na kusababisha vifo hivyo pia wanafunzi watatu wa shule ya sekondari Jihadi pia wamejeruhiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news