Mwanafunzi wa Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari ya UWC East Africa ya jijini Arusha,Aalaa Riyaz Somji ameibuka mshindi wa jumla katika mashindano ya Gofu ya “Diplomatic Golf 2020“ yaliyofanyika katika uwanja wa mchezo huo wa Kili Golf uliopo Usa River jijini humo, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Mbali na ushindi huo Aala mwenye umri wa miaka 17 pia ameibuka mshindi
wa kwanza wa mchezo huo kwa upande wa wanawake huku akijinyakulia zawadi
ya saa pamoja na mapumziko ya siku tatu katika Hoteli ya Manta Resort
pamoja na kulala usiku mmoja kwenye chumba kilichopo chini ya bahari.
Mashindano ya Diplomatic Golf 2020 yaliyodhaminiwa na Benki ya CRDB yameshirikisha washiriki zaidi ya 150 kutoka mataifa 19 yamefanyika kwa mara ya pili sasa yakilenga kuwakutanisha wanadiplomasia ,watendaji wakuu wa makampuni ,wafanyabiashara wakubwa na wachezaji mbalimbali wa gofu ambao hawashiriki mashindano ya kitaifa na kimataifa.

Mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume ameibuka Tender Singh Bansal aliyejinyakulia kiasi cha shilingi milioni moja kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo ambao ni Benki ya CRDB,fedha ambazo hata hivyo alizitoa kwa taasisi isiyo ya kiserikali ya SIMO ya Songea kwa ajili ya kusaidia watoto waishio kwenye mazingira magumu. |
Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi ,mgeni rasmi
katika mashindano hayo aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Damas Ndumbaro amesema mashindano hayo yametumika katika kutekekleza diplomasia
ya kiuchumi kwa vitendo.
“Tumekutanisha makundi yote haya pamoja wacheze mpira wa Gofu wafurahi,lakini muhimu zaidi waongee masuala ya ushirikianao wa kiuchumi,yaani kupitia mashindano kama haya tunatekeleza Diplomasia ya kiuchumi kwa vitendo,"amesema Ndumbaro.
Ndumbaro amesema kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika mashindano ya mwaka huu akatangaza rasmi uwanja wa Gofu wa Kili Golf uliopo Usa River jijini Arusha kuwa nyumbani mwa mashindano ya “Diplomatic Golf” na kwamba mwakani pia yatafanyika katika viwanja hivyo.

Mshindi wa jumla katika mashindano ya Gofu ya Diplomatic Golf 2020,Aalaa Riyaz Somji akionesha zawadi zake mara baada ya kukabidhiwa kutokana na kuongoza kwenye mashindano hayo yaliyofanyika katika viwanja vya mchezo huo vya Kili Golf vilivyopo Usa River jijini Arusha.
Meneja Mwandamizi wa Huduma ya Premier katika Benki ya CRDB, Gibson Mlaseko (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya kiasi cha shilingi milioni moja kwa mshindi wa kwanza katika mashindano ya Gofu ya "Diplomats Golf 2020", Tender Singh Bansal (wa pili toka kulia) baada ya kuibuka mshindi kwa upande wa wananume katika mashindano yaliyofanyika katika viwanja vya Gofu vya Kili Golf jijini Arusha.Wengine ni Simon Travern na Prosper Nambaya.
“Sasa naweza kutangaza rasmi kwamba “Kili Golf is a home of Diplomatic Golf” ,tutakuwa na siku mbili na hii ni baada ya kukataa maombi ya washiriki wengine kutokana na idadi ya wachezaji tuliyokuwa tumejiwekea,"amesema Ndumbaro.
Wadhamini wa mashindano hayo Benki ya CRDB kupitia Meneja wa Huduma ya Primier, Gibson Mlaseko amesema kama CRDB wataendelea kusaidia michezo mbalimbali kwa kuwa ni sehemu ya jamii na inawezesha mashirikiano na kuboresha mahusiano baina yao.
Meneja Mwandamizi wa Huduma ya Premier katika benki ya CRDB, Gibson Mlaseko (wa pili kushoto) pamoja na Prosper Nambaya wakishirikiana na nahodha wa mchezo wa Gofu wa klabu ya Kili ya jijini Arusha, Simon Travern wakikabidhi mfano wa hundi ya kiasi cha shilingi moja kwa Mwenyekiti wa taasisi isiyo ya kiserikali ya SOMI ya Songea,Nathani Mpangala kwa ajili ya kusaidia watoto waishio kwenye mazingira hatarishi.
Meneja Mwandamizi wa Huduma ya Premier katika Benki ya CRDB, Gibson Mlaseko akijiandaa kupiga mpira wake wa kwanza wakati wa mashindano ya Diplomatic Golf yaliyofanyika katika viwanja vya Gofu vya Kili Golf jijini Arusha.
Mchezaji wa Gofu kutoka klabu ya Gofu ya Moshi,George Nyagabona akijiandaa kupiga mpira wake wa kwanza katika mashindano ya mchezo huo ya Diplomatic Golf yaliyofanyika katika viwanja vya Kili Golf jijini Arusha.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt.Edmund Mdolwa akipiga mpira katika mashindano ya Diplomatc Golf yaliyofanyika jijini Arusha. .Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mstaafu, Dkt.Damas Ndumbaro akipiga mpira wa mwisho katika shimbo namba 18 wakati akihitimisha mzungungo katika mashindano ya Gofu ya Diplomatic Golf 2020 yaliyofanyika katika viwanja vya Gofu ya Kili Golf jijini Arusha.
Naibu Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza muda mfupi baada ya zawadi kukabidhiwa kwa washindi wa mashindano ya Gofu ya Diplomatic Golf 2020 yaliyofanyika katika viwanja vya Gofu ya Kili Golf jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wa mashindano hayo wakifuatilia matukio mbalimbaliyaliyokuwa yakiendelea katika eneo la Club House.
Baadhi ya washiriki wa mashindano hayo wakifuatilia matukio mbalimbaliyaliyokuwa yakiendelea katika eneo la Club House.
Meneja Mwandamizi wa huduma ya Premier katika benki ya CRDB, Gibson Mlaseko akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhi zawadi ya kiasi cha shilingi milioni moja kwa washindi wawili wa kwanza katika mashindano ya Mchezo wa Gofu ya Diplomatic Golf 2020.
Washindi waliofanikiwa kupata zawadi mbalimbali katika mashindano ya Gofu ya Diplomatic Golf 2020 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao. Mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya sekondari ya UWC East Africa ya jijini Arusha,Aalaa Riyaz Somji ameibuka mshindi wa jumla katika mashindano ya Gofu ya “Diplomatic Golf 2020 “yaliyofanyika katika uwanja wa mchezo huo wa Kili Golf uliopo Usa River Arusha.
“Gofu inatazamwa kama ni mchezo wa watu matajari peke yake, lakini sisi kama CRDB tunaendelea kuwaalika na watu wengine kushiriki katika mchezo huu lakini pia kama CRDB tumeweka nguvu yetu katika mashindano haya kwa sababu seheumu ya mapato yanayopatikana katika tukio hili yanaenda kusaidia sehemu ya jamii ya watoto huko Songea,"amesema Mlaseko.
“Tumeona ni jambo zuri kuwa sehemu ya msaada kwa jamii hii lakini pia tumetoa zawadi kwa wachezaji wawili walioweza kufanya vizuri katika mashindano haya hadi kiasi cha shilingi milioni moja fedha ambazo wameomba ziende kutumika usaidia watoto huko Songea,”AMEongeza Gibson.
Shindano la kwanza la mchezo wa Gofu la Diplomatic Golf lilifanyika mwaka jana Zanzibar katika viwanja vya Gofu Sea Clif huku la pili likifanyika katika viwanja vya Kili Golf jijini.