Ndugai, Tulia wajitosa kutetea nafasi zao Bungeni

Siku moja baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoa tangazo la kuwaita wanaotaka kuwania nafasi za Uspika, Unaibu Spika, Umeya na Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya, Novemba 3,2020 baadhi ya wanachama wa chama hicho wameonyesha nia na tayari wamechukua fomu, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Miongoni mwao katika nafasi ya Uspika na Unaibu Spiaka ndani ya chama hicho ni aliyekuwa Spika wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Job Ndugai na Naibu wake, Dkt.Tulia Ackson ambao wamejitokeza jijini Dodoma kuchukua fomu za kuwania nafasi hizo. 
Ndugai ambaye ni Mbunge Mteule wa Jimbo la Kongwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amewania nafasi ya Uspika huku akiwaomba Watanzania wamuombee ili chama chake kimteue tena kuwa mgombea wa nafasi hiyo katika Bunge lijalo. 

“Nafasi ya Spika inapendekezwa na vyama vya siasa, hivyo ikiwa chama changu kitanikubalia kuwa Spika wa Bunge la 12 tutaongea na Watanzania kwa wakati huo juu ya vipaumbele vyetu,"amesema Ndugai.

Aidha,Katibu Msaidizi Mkuu wa Oganaizesheni Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Solomon Itunda amesema zoezi hilo limeanza rasmi Novemba 3,2020 huku akimtaja Spika anayemaliza muda wake Job Ndugai kuwa ndiye mgombea pekee wa nafasi hiyo ambaye amekamilisha taratibu zote. 

Pia amesema,gharama za fomu hizo ni sh. 500, 000 kwa kila fomu huku kwa upande wake Dkt.Tulia ambaye ni Mbunge Mteule wa Mbeya Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuchukua fomu amesema kuwa,iwapo atateuliwa kuongoza nafasi hiyo atahakikisha anawasimamia wabunge ili waweze kuwawakilisha wananchi wao kwa usahihi huku akiwataka wabunge kujenga desturi ya kusoma kanuni ili wazielewe zinataka nini.
“Bungeni kuna namna yake ya kukaa, kuongea na jinsi ya kuwawakilisha wananchi,nitoe wito kuwa wabunge wanapofika bungeni inabidi wajifunze kanuni za Bunge na kuzielewa kwa sababu pale kuna namna ya kuzungumza, kukaa na jinsi ya kuwakilisha hoja za wananchi wa majimbo yao,” amesema Dkt.Tulia Ackson huku akisisitiza yeye ni mwanamke jasri ambaye huwa hana hofu wala uoga wa kuwania nafasi yoyote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news