Tanzania imezidi kung'ara katika uga wa Kimataifa, baada ya jarida la Forbes kuitaja kuwa ni nchi ya pili duniani inayofaa kutembelewa zaidi mwaka 2021, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kwa mujibu wa jarida hilo, Tanzania ipo namba mbili kati ya nchi zilizopo katika orodha ya nchi 21 duniani zenye maeneo mazuri zaidi ya kutembelewa kwa mwaka huo.
Taifa la Maldives ambalo ni kisiwa kidogo kilichopo kwenye bahari ya Hindi imetajwa ya kwanza kwenye orodha hiyo, na Tanzania hasa mbuga ya wanyama ya Serengeti imetajwa kuwa ya pili inayofaa kutembelea zaidi.
Kwa mujibu wa jarida hilo, nchi nyingine ya Afrika Mashariki iliyopo kwenye eneo hilo ni Rwanda ambayo iko kwenye nafasi ya saba.
Aidha, orodha ya kumi bora ni pamoja na 1. Maldives 2. Tanzania (Serengeti) 3. Antarctica, 4. Ziwa Powell katika jimbo la Utah Marekani, 5 Bonde la Jackson, Wyoming 6.Cucso Peru, 7. Rwanda 8. 8. Denali National Park, Alaska 9. Porto Cervo, Italy 10. Sonoma County, California.
Haya ni mafanikio makubwa kwa Taifa la Tanzania ambalo linataka kuvuka uchumi wa kati kupitia rasilimali zake za asili ambazo zimewezesha mafanikio makubwa kwa miaka michache iliyopita.
Tags
Habari