Nini wanaongea kuhusu simu ya TECNO SPARK 5PRO

TECNO Spark 5 pro ilizinduliwa rasmi Oktoba 18, 2020 ambapo wakati wa uzinduzi huo, ilikutanisha wadau wa simu za TECNO na wasanii mbalimbali akiwemo mchekeshaji maarufu Eric Omondi na DJ Maphorissa kutoka Afrika Kusini.
Tangu kuzinduliwa kwa simu hiyo imekuwa ni neema kwa watumiaji wa simu za Spark. TECNO Spark 5pro imeonekana kukonga mioyo ya watu wengi hasa kutoka na uwezo wake wa kuhifadhi 'files' nyingi pasipo uhitaji wa 'memory' ya ziada.

Spark 5pro inaukubwa wa memory ya GB 64ROM + GB 3RAM. Sifa nyingine za TECNO Spark 5pro ni uhimili wake wa kudumu na chaji kwa muda mrefu kutokana na batri yake kuwa na ujazo wa mAh 5000.

Kwa wapenzi wa picha kali Spark 5pro ni suluhisho kwao, Spark 5pro imekuja na selfie ya megapixel 8 na nyuma in megapixel 16M+2M+2M+AI Lens za kamera.

Kama ilivyo ada, mcheza kwao hutunzwa na ndivyo ilivyo kwa Spark 5pro si mitandaoni tu bali hata kwa wenye maduka wamekuwa na mazuri ya kuzungumza kuhusiana na simu ya TECNO Spark 5pro.

“Spark 5pro ni kama baba kwenye familia bila yeye mambo hayaendi basi ndivyo ilivyo kwa simu hiyo sokoni kwa sasa haiwezi pita siku pasipo simu 10 za Spark 5 pro kuuzika dukani,”amesema mfanyabiashara maarufu aliyejitambulisha kwa jina la Patel Kanjibai.

“Spark 5pro ni mkombozi kwetu sisi wanafunzi, simu hii inamambo mengi mazuri sana napenda kasi yake ya kimtandao wa 4G, kasi ya processor 1.8 octa-core na mfumo wa uendeshaji wa Android 10,” amesema mwanafunzi wa Chuo cha IFM, Bw. Frank Peter.
Baada ya huu uchunguzi inaonyesha kampuni ya simu TECNO imefaulu kwa asilimia 100 kwenye toleo hili la Spark 5pro.

Ili kufurahiya huduma za TECNO Spark 5pro tafadhali usiache kuwatembelea katika maduka yao ya TECNO Smart Hub Kariakoo na Mlimani City, lakini pia tembelea link https://bit.ly/2Hftrh6 hii kufahamu mengi mazuri kutoka TECNO.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news