Paz asema atamchapa makonde ya nguvu Mwakinyo

Bondia Jose Carlos Paz atakayezichapa na Hassan Mwakinyo Novemba 13, 2020 kwenye ukumbi wa Next Door Arena Oysterbay jijini Dar es Salaam amewasili na kutamba kutwaa ubingwa wa uzito wa Weight Super Welter (WBF) unaoshikiriwa na Hassan Mwakinyo, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Paz amewasili na baba yake Alberto Ramon Paz ambaye pia ni kocha wake kama ilivyo kwa bondia Floyd Mayweather. Akizungumza mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam Paz amesema kuwa, amesafiri umbali mrefu kwa ajili ya kutwaa ubingwa katika pambano hilo linalojulikana kwa jina la Jackson Group Fight Night.
Bondia Jose Carlos Paz wa Argentina (wa pili kulia) akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA terminal 3) tayari kwa pambano la ubingwa wa uzito wa Weight Super Welter (WBF) dhidi ya bingwa mtetezi Hassan Mwakinyo Novemba 13, 2020 kwenye ukumbi wa Next Door Arena Oysterbay jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni baba yake, Ramon Paz ambaye pia ni kocha wake. Wengine katika picha ni Don Hala wa Jackson Group Sports (wa kwanza kushoto) na wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC), Yahya Poli.

Paz amesema kuwa, amechukua tahadhari kubwa kwa ajili ya Mwakinyo na kwamba siyo bondia mbaya. “Nimefika mapema zaidi ili kuzoea hali ya hewa, hii ni moja ya mikakati ya ushindi, nilisafiri kwa basi na baadaye kupanda ndege, siku mbili nipo njiani, sitakuwa tayari kushindwa katika pambano hili,”amesema Paz.

Kocha wake, Alberto Ramon naye amesema kuwa, wamemsoma Mwakinyo katika mapambano yake na kujua mbinu zake ambazo amezifanyia kazi. “Tumefanya mazoezi magumu kuelekea pambano hili, tumefanya mazoezi ya ufundi na mbinu, hayo yote ni kwa ajili ya kusaka ushindi ambao tunaamini asilimia 100, tutashinda,”amesema Ramon. Mwakinyo afanya zoezi kali kumchapa Paz.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jackson Group Sports, Kelvin Twissa amesema maandalizi yanaendelea vizuri na mabondia wa Zambia, Zimbabwe na Kenya watawasili wiki ijayo kwa ajili ya pambano hilo. Twissa amesema, kila kitu kipo katika hatua za mwisho na tiketi zitaanza kuuzwa kwa njia ya Nilipe na Selcom kwa shilingi milioni tatu kwa meza ya watu 10 na sh. 150,000 kwa kwa viti vya kawaida.

Pambano hilo litatanguliwa na mengi matatu ambapo bondia nyota wa kike nchini, Zulfa Macho atazipiga na Alice Mbewe kutoka Zambia, Hussein Itaba atazichapa na Alex Kabangu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Fatuma Zarika wa Kenya atacheza na Patience mastara wa Zimbawe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news