Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo Novemba 30,2020 saa 10 jioni anatarajiwa kuwaapisha wabunge wawili walioteuliwa na Rais Dkt.John Magufuli akiwemo Humphrey Polepole ambaye ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM na Riziki Said aliyekuwa Mbunge Viti Maalum katika Bunge la 11 kupitia Chama cha Wananchi (CUF).