Rais avunja Bodi ya Mitihani kwa kuvujisha mitihani

Rais wa Malawi, Dkt.Lazarus Chakwera ameagiza Bodi ya Mitihani ya Kitaifa nchini Malawi (MNEB) kuvunjwa baada ya mitihani ya kitaifa ya mwaka huu kuvuja na kusambaa katika mitandao ya kijamii kabla ya watahiniwa kuifanya.

Hatua ya mitihani hiyo kuvuja, ilipelekea mitihani ya kitaifa kuahirishwa na kupelekea wanafunzi kuingia mitaani kwa maandamano, wakikabiliwa na polisi waliowatawanya kwa kutumia gesi ya kutoa machozi.

Rais Lazarus Chakwera akihutubia Taifa amesema kwamba, wasimamizi wa bodi ya mitihani nchini humo wanastahili kufutwa kazi kwa kuzembea kazini na kupelekea mitihani ya kitaifa kuvuja.

Agizo hilo linajiri baada ya Wizara ya Elimu kufutilia mbali mtihani wa kitaifa kwa watahiniwa wa shule za upili, uliokuwa umepangiwa kuanza Oktoba 27,mwaka huu.

Rais Chakwera amesema kwamba hatua ya mitihani hiyo kuvuja ni dhihirisho kwamba bodi inayosimamia mitihani ya kitaifa haina uwezo wa kusimamia mitihani nchini humo.

Polisi wamekamata wanafunzi 38 na walimu watatu kutoka shule baada ya kupatikana na karatasi sita za mitihani zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Mkurugenzi wa MNEB,Gerald Chiunda aliwaeleza waandishi wa habari kuwa,huenda karatasi za mitihani zilivuja kutoka ofisini mwake na kwamba uchunguzi unaendelea.

Rais Chakwera ameamuru Waziri wa Elimu kuwaadhibu wahusika wote kabla ya mwezi huu wa Novemba kukamilika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news