Rais Dkt. Hussein Mwinyi amuapisha Katibu wa Rais Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemuapisha Suleiman Ahmeid Saleh kuwa Katibu wa Rais wa Zanzibar, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Hafla hiyo ya kiapo imefanyika leo Novemba 7, 2020 Ikulu jijiji Zanzibar. Rais Dkt. Mwinyi amemuapisha Katibu huyo baada ya kumteua Novemba 4, mwaka huu kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 53 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akimuapisha,   Bw.Suleiman Ahmed Saleh kuwa Katibu wa Rais wa Zanzibar hafla iliyofanyika  leo Novemba 7, 2020 ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar. Kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi pia Katibu Kiongozi , Dkt.Abduhamid Yahya Mzee.[Picha na Ikulu/ Diramakini].

Katika hafla hiyo viongozi mbalimbali walihudhuria akiwemo Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi Talib Haji, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Hassan Khatib, Naibu Kadhi Mkuu Sheikh Hassan Othman Ngwali, viongozi wa Vikosi vya SMZ pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Idara na taasisi mbalimbali za Serikali. Kabla ya uteuzi huo Katibu huyo alikuwa Mkurugenzi Msaidizi katika Tume ya Pamoja ya Fedha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news