Rais Dkt. Mwinyi amteua Makamu wa Pili wa Rais

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi leo Novemba 8, 2020 amemteua Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

  

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,anaripoti Mwandishi Diramakini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee ilieleza kwamba Rais Dkt. Hussein Mwinyi amemteua Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa mujibu wa uwezo aliyopewa chini ya Kifungu Namba 39 (1) na 39 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Kabla ya Uteuzi huo Hemed Suleiman Abdulla alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.Uteuzi huo umeanza leo Novemba 8, 2020.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdalla  aliyeteuliwa leo Novemba 8, 2020 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news