Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akimuapisha, Rashid Said Rashid kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayeshuhulikia masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar. |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akitia saini hati ya kiapo ya Rashid Said Rashid mara baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayeshuhulikia masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar. |
Katika
maelezo yake mara baada ya kula kiapo Naibu Katibu Mkuu huyo ambaye pia
atakuwa anashughulikia masuala ya fedha na kodi amesema kwamba,
wananchi wana matumaini makubwa na mabadiliko kwani wanahitaji kupata
huduma nzuri na zilizo bora zaidi.
Amesisitiza kwamba, teknolojia
ya TEHAMA haitokuwa kwenye kodi pekee yake na badala yake itakwenda
kwenye kila sekta ikiwemo uchumi wa buluu, huduma za afya, elimu na
nyinginezo.
Aidha, amesema kuwa ipo haja ya kutumia teknolojia
katika kutatua matatizo ya walimu na kusema kwamba Chuo Kikuu cha Taifa
cha Zanzibar (SUZA) kina uwezo mkubwa wa kufanya hivyo, lakini kwa
kuanzia alisema kuwa hatua hiyo itaanza katika ukusanyaji wa kodi kama
alivyosisitiza Rais Dkt.Mwinyi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimkabidhi hati ya kiapo, Rashid Said Rashid mara baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayeshuhulikia masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiagana na Rashid Said Rashid mara baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayeshuhulikia masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika hafla iliyofanyika leo Novemba 24, 2020 katika Ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Amesema kwamba, lengo la Serikali
ni kuhakikisha wananchi wanalipa kwa urahisi zaidi na kuepuka wananchi
kwenda kulipa benki na kukaa muda mrefu, hivyo ni lazima mifumo ya awali
iondolewe ikiwa ni pamoja na kupata wepesi katika kufuatia masuala ya
vyeti vya kuzaliwa.
Ameongeza kwamba, Serikali itajipanga katika
kuhakikisha wahitimu wa vyuo vya Zanzibar wanapata muelekeo kwa
kuwatumia hapa hapa nchini na hakuna haja ya kuwaita wataalamu kutoka
nje jambo ambalo litafanywa haraka iwezekenavyo ili kuondoa tatizo la
walimu hasa wa sayansi. Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayeshuhulikia masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Rashid Said Rashid (kutoka kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango, Jamal Kassim Ali,Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Kiongozi, Dkt.Abduhamid Yahya Mzee,Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali na Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume. (Picha na Ikulu).
Naibu Katibu Mkuu huyo alitangazwa siku
ya Jumanne ya Novemba 22, 2020 ambapo Rais Dkt.Mwinyi alifanya uteuzi
huo kwa mujibu wa kifungu cha 50(4) cha Katiba ya Zanzibar.
Kabla
ya uteuzi huo Naibu Katibu Mkuu huyo alikuwa Mkurugenzi wa Mifumo ya
Teknolojia ya Habari na Mawasilino (TEHAMA) katika Benki Kuu ya
Tanzania, ambapo uteuzi wake ulianza rasmi Novemba 23, mwaka huu.