Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua, Suleiman Ahmed Salum kuwa Katibu wa Rais. Hayo yamethibitishwa leo Novemba 4,2020, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee kabla ya uteuzi huo, Suleiman Ahmed Salum alikuwa Mkurugenzi Msaidizi katika Tume ya Pamoja ya Fedha.
Uteuzi huo ameufanya Dkt.Hussein Mwinyi kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 53 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Wakati huo huo, Rais Dkt.Hussein Mwinyi kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 6(1) cha Sheria ya Shirika la Bandari Namba 1 ya mwaka 1997 amemteua Nahaat Mohammed Mahfoudh kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar. Kabla ya uteuzi huo, Nahaat Mohammed Mahfoudh alifanya kazi katika taasisi mbalimbali za sekta binafsi ambao uteuzi huo umeanza leo Novemba 4,2020.