Rais Dkt.Hussein Mwinyi amuapisha Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemuapisha Dkt. Mwinyi Talib Haji kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

Hafla hiyo ya kiapo imefanyika leo Ikulu jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, viongozi wa Idara Maalum za SMZ, viongozi wa Serikali pamoja na wanafamilia.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Dkt. Mwinyi Talib Haji kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

Rais Dkt. Mwinyi amemuapisha Mwanasheria huyo baada ya kumteua Novemba 3, mwaka huu kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu Namba 55 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Haji alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news