Rais Dkt.Mwinyi ateua Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi akiwemo Saada Mkuya Salum

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa Wajumbe wanne wa Baraza la Wawakilishi, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Wajumbe hao walioteuliwa na Rais Dkt. Hussein Mwinyi ni Saada Mkuya Salum, Tabia Maulid Mwita, Juma Ali Khatib na Hemed Suleiman Abdalla.

Mheshimiwa Saada Mkuya Salum.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee ilieleza kwamba Rais Dkt. Hussein Mwinyi amewateua Wajumbe hao wa Baraza la Wawakilishi kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 66 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Taarifa hiyo imeeleza kwamba, uteuzi huo umeanza leo Novemba, 2020. Aidha, viongozi hao waliotajwa wametakiwa kuripoti Baraza la Wawakilishi Novemba 8, 2020 saa 6.00 mchana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news