Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemteua, Prof. Adelardius Lubango Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeeleza kuwa, uteuzi wa Prof. Kilangi umeanza Novemba 5,2020.
Prof. Kilangi ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika Novemba 5, 2020.
Tags
Habari