Rais Magufuli awatoa hofu Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewatoa hofu Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwani ameanza nao na atamaliza nao, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Rais Magufuli amesema hayo katika hafla ya kumwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilangi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Chamwino jijini Dodoma.
“Mkuu wa mkoa unakuwa na wasiwasi gani labda kama ulikuwa ufanyi kazi vizuri kwasababu nashangaa napata vimesji vingine Mhe Rais nimejitahidi katika kipindi changu kana kwamba kipindi chake nilimwambia kinaisha baada ya mimi kuapishwa nimeona hili nilizungumze kwamba Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya msiwe na wasiwasi,"amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema kuwa, kunaweza kusitokee mabadiliko katika nafasi hizo isipokuwa kwa mtu anayestaafu au atakayefanya mambo ya hovyo, “kwa nini nibadilishe Mkuu wa mkoa, kwanini nibadilishe mkuu wa Wilaya, kwanini nibadilishe Mkurugenzi, kwanini nibadilishe DAS Serikali ni ile ile,”amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amewataka watendaji hao kuchapa kazi kwani anajua alianza nao na atamaliza nao, ameongeza kuwa hata kwa watendaji wengine akitolea mfano Makatibu Wakuu nao itakuwa hivyo hivyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

Previous Post Next Post

International news