Rais Ouattara ashinda urais kwa asilimia 94.3

Rais wa Ivory Coast, Alassane Dramane Ouattara ameshinda mhula wa tatu madarakani kwa asilimia 94.27 ya kura, ushindi ambao unatajwa kuwa mkubwa zaidi, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mwanasiasa huyo wa Ivory Coast ambaye alizaliwa Januari Mosi, 1942 ambapo kwa sasa ana umri wa mika 78 alianza muhula wake wa kwanza mwaka 2010 huku wapinzani wakisusia uchaguzi huo kwa madai kuwa ulikuwa batili na wameunda Serikali yao mbadala.

Aidha, wanasiasa wakuu wa upinzani wanakabiliwa na kesi mahakamani baada ya kususia uchaguzi wa Oktoba 31, mwaka huu na kuunda Serikali yao.

Rais Ouattara amesema kwamba, yupo tayari kwa mazungumzo na wanasiasa wa upinzani ili kutuliza joto la siasa katika nchi hiyo ambayo inazalisha kiwango kikubwa cha Cocoa duniani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news