Rais wa Mexico akataa kumpongeza Joe Biden

Rais wa Mexico, Andres Manuel Lopez Obrador amesema hawezi kumpongeza mshindi wa urais wa uchaguzi wa Marekani, Joe Biden mpaka taratibu za kisheria zitakapohitimishwa,anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mheshimiwa Obrador amesema,msimamo wake huo ni wa busara za kisiasa na hawezi kumpongeza mgombea mmoja au wagombea hadi mchakato wa uchaguzi uishe.
Rais Andres Manuel Lopez Obrador wa Mexico.

"Kwa heshima ya uchaguzi wa Marekaini, tutasubiria hadi pale taratibu za kisheria zitakapohitimishwa. Siwezi kumpongeza mgombea mmoja au mwingine. Hadi pale ambapo mchakato wa uchaguzi utakamilika,"amesema Rais Andres Manuel Lopez Obrador katika mkutano na waandishi wa habari nchini Mexico.

Mexico ni mshirika mkubwa wa kibiashara na Marekani ambaye kwa mwaka wanafanya biashara ya zaidi ya dola bilioni 600 huku mahusiano ya pande hizo mbili yakitajwa ni muhimu katika mataifa hayo hususani Kaskazini ambapo ni eneo muhimu kwa Mexico.

Uamuzi huo unakuja baada ya Novemba 7, 2020, Joe Biden kutangazwa kuwa rais mteule wa Marekani, kufuatia ushindi wake katika jimbo la Pennsylvania ambao ulimfanya apate kura za wajumbe maalum zaidi 270 zinazohitajika. 

Hata hivyo, Rais Donald Trump ameanzisha mchakato wa kisheria kupinga matokeo hayo, ingawa maafisa wa uchaguzi katika majimbo tofauti ya Marekani wanasema hakuna ushahidi wa maana wa udanganyifu na wataalamu wa sheria pia wakisema juhudi za Trump haziwezi kufanikiwa kwa sasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news