Rwanda yaongoza Duniani kwa mikakati ya usawa wa kijinsia

Rais mteule wa Marekani Joe Biden, ameahidi kuteua baraza la mawaziri ambalo ametaja kama lenye uwiano mzuri huku akiahidi kuwateua wanawake kadhaa katika serikali yake.

Kwa mujibu wa VOA, Biden amemteua, Avril Haines kuwa mkuu wa idhara ya ujasusi wa kitaifa na Janet Yellen kama waziri wa fedha. Ni wanawake wa kwanza kuteuliwa katika nafasi hizo.

Ahadi ya Biden ya kuwa na serikali yenye usawa wa kijinsia inafuatia mifano kadhaa katika serikali mbalimbali duniani.Ifuatayo ni orodha ya nchi 7 zinazoongoza kwa usawa wa kijinsia serikalini.

Rwanda

Rwanda, ambayo ni nchi ndogo ya Afrika Mashariki, inajivunia kwa sifa kubwa ya kuwa na idadi kubwa ya wanawake katika nafasi za kisiasa na serikalini.

Karibu theluthi tatu ya wabunge na asilimia 52 ya mawaziri ni wanawake. Spika wa bunge chini ni mwanamke.Wizara za habari na mawasiliano, biashara na viwanda zinaongozwa na wanawake.

Katiba ya Rwanda iliyoandikwa mwaka 2003, baada ya vita vya kimbari vya mwaka 1994 inatoa fursa kwa wanawake wengi kushiriki katika siasa, ikitaka asilimia 30 ya viti vya kisiasa kutengewa wanawake.

Wakati wa maadimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake mwaka 2020, rais wa Rwanda Paul Kagame aliandika ujumbe wa twiter kwamba “kila wakati wanawake wanafanikiwa, nchi nzima inafanikiwa maendeleo hayawezi kupatikana bila ya kuwepo usawa wa kijinsia.”

Ethiopia

Ethiopia ni nchi ya pili yenye idadi kubwa ya watu Afrika. Imechukua hatua madhubuthi kuimarisha usawa wa kijinsia katika uteuzi wa maafisa serikalini tangu waziri mkuu Abiy Ahmed alipoingia madarakani mwaka 2018.

Aliyekuwa mwanadiplomasia Sahle-Work Zewde alichaguliwa kuwa rais Octoba 2018 na kuwa mwanamke wa kwanza kushikilia nafasi hiyo nchini humo.

Meaza Ashenafi aliteuliwa kuwa jaji mkuu mwezi Novemba mwaka 2018.

Asilimia 45 ya mawaziri katika serikali ya Abiy Ahmed ni wanawake.

Wizara za uchukuzi, maendeleo ya mijini na ujenzi zinaongozwa na wanawake.

Canada

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Canada, baraza la mawaziri lilipata idadi sawa ya wanawake na wanaumme miaka 5 iliyopita, waziri mkuu Justin Trudeu alipoanzisha utawala wa usawa wa jinsia.

Baraza la mawaizi lina wanawake 18 na wanaumme 18.

Naibu wa waziri mkuu ambaye pia ni waziri wa fedha Chrystia Freeland, ni mwanamke.

Colombia

Rais wa Colombia Ivan Duque alipoingia madarakani mwaka 2018, aliteuwa idadi sawa ya wanawake na wanaumme katika baraza la mawaziri. Hatua hiyo ilikuwa ya kwanza kuwahi kutokea nchini humo, ambapo kwa mara ya kwanza, mwanamke aliteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani.

Kwa sasa, wanawake sita wanaongoza wizara mbalimbali kati ya baraza lake la mawaziri 16.

Marta Lucia Ramirez ni mwanamke wa kwanza kuwa makam war ais nchini Colombia.

Afrika kusini

Mnamo mwezi Juni 2019, rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa alisifiwa alipoteua baraza lake la mawaziri ambalo asilimia 47 ni wanawake, ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo. Wizara 14 kati ya 28 zinaongozwa na wanawake.

Japo kuwa wanaokosoa kwamba nafasi za juu kama rais na naibu wake zimeshikiliwa na wanaumme, kuna wanaosema kwamba uteuzi wa Ramaphosa ni hatua nzuri nay a kuleta matumaini ya kupatikana usawa wa jinsia nchini Afrika kusini.

Iceland

Iceland in historia ya kuchagua wanawake kuwa kiongozi wa serikali, tangu mwaka 1980 wakati Vigdís Finnbogadóttir alipokuwa rais.

Alikuwa madarakani hadi mwaka 1996. Iceland imeongozwa na wanawake kwa miaka 22 katika miaka 50 iliyopita. Kati ya wizara 10 katika serikali ya nchi hiyo ndogo, zinaongozwa na wanawake, ikiwemo wizara ya haki.

New Zealand

Waziri mkuu wa sasa Jacinda Arden, alishinda uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba kwa kishindo. Bunge la New Zealanda lina idadi kubwa ya wanawake.

Baraza la mawaziri lenye mawaziri 20, lina wanawake 8. Nanaia Mahuta ni mwanamke wa kwanza kuwa waziri wa mambo ya nje wa New Zealand.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news